DKT. SAMIA AENDELEZA KAMPENI SONGWE, AWAHUTUBIA WANANCHI WA MLOWO

 




Na mwandishi wetu

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 4, 2025 amezungumza na wananchi wa Mlowo, mkoani Songwe.

Dkt. Samia, akiwa njiani kuelekea Mbalizi mkoani Mbeya, aliwahakikishia wananchi kuwa serikali ya CCM itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma za kijamii, kukuza uchumi wa wananchi na kulinda amani ya taifa.

Katika mkutano huo wa kampeni, wananchi walijitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza, ambapo alisisitiza dhamira ya chama hicho kuendeleza miradi ya kimkakati, ikiwemo sekta za afya, elimu, barabara, nishati na kilimo.

Aidha, aliwaomba wananchi waendelee kuiamini CCM kwa kumpa kura za ushindi ifikapo Oktoba 29, 2025, pamoja na kuwapigia kura wagombea wa ubunge na udiwani kupitia chama hicho.













Post a Comment

0 Comments