DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KAMPENI ZA CCM MKOANI DODOMA

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 09 Septemba 2025 ameendelea na kampeni za chama hicho mkoani Dodoma kwa kukutana na wananchi wa Bahi.

Katika mkutano huo wa hadhara, Dkt. Samia aliwasalimia maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea, akiwashukuru kwa mapokezi makubwa na kuahidi kuendeleza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita

Aidha, alisisitiza dhamira ya CCM kuimarisha huduma za kijamii, ikiwemo elimu, afya, maji safi na uboreshaji wa miundombinu, hasa barabara na umeme vijijini.

Mkutano huo ni sehemu ya muendelezo wa kampeni za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ambapo Dkt. Samia ameendelea kusisitiza mshikamano, umoja na amani kama nguzo kuu za maendeleo ya Taifa.

Wananchi wa Bahi walionyesha ari kubwa ya kuunga mkono CCM kwa shangwe, nyimbo na mabango, wakiahidi kumpa kura za kishindo ili aendelee kuongoza Tanzania.







Post a Comment

0 Comments