MATUKIO YA KAMPENI ZA CCM UWANJA WA BOMBADIA SINGIDA

 





Na Mwandishi Wetu

Singida, 09 Septemba 2025


Matukio mbalimbali yamejiri katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Uwanja wa Bombadia, mkoani Singida, tarehe 09 Septemba 2025.

Mkutano huo ulivuta umati mkubwa wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Singida na mikoa jirani waliokusanyika kumsikiliza mgombea urais kupitia CCM pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.

Katika mkutano huo, viongozi wa CCM walipata nafasi ya kueleza mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya CCM, huku wakiahidi kuendeleza jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi.

Viongozi mbalimbali walizungumza wakihimiza mshikamanano, amani, na mshiriki mkubwa wa wananchi katika uchaguzi ujao wa tarehe 29 Oktoba 2025.

Wananchi waliimba nyimbo za hamasa na kushangilia kwa furaha, wakionesha imani na mshikamano wao na chama hicho. Aidha, tukio hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa vikundi vya ngoma za asili na wasanii wa kizazi kipya waliotoa burudani ya aina yake.

Mkutano wa Singida umeelezwa kuwa ni sehemu ya mwendelezo wa mikutano ya kampeni ya CCM inayofanyika nchi nzima kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.











Post a Comment

0 Comments