📍 Igunga – Tabora
🗓️ 10 Septemba 2025
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepanga kujenga soko kubwa na la kisasa katika mji wa Igunga, wilayani Tabora, lengo likiwa kuhakikisha wafanyabiashara wa aina zote wanapatikana katika eneo moja. Soko hili jipya litarahisisha upatikanaji wa bidhaa kwa wananchi na pia kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Aidha, Rais Dkt. Samia ameahidi kujenga stendi mpya ya kisasa ndani ya mji wa Igunga, yenye hadhi ya juu, ambayo itawawezesha wageni kutoka mikoa jirani na wafanyabiashara wadogo na wakubwa kufikiwa kwa urahisi. Uwepo wa soko na stendi hii unatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha uchumi wa mkoa wa Tabora.
#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi
#KaziNaUtuTunasongaMbele
0 Comments