Na mwandishi wetu
Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaeleza Watanzania kuwa CCM ina mipango mikubwa na thabiti katika kuchochea maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni na maelfu ya wananchi wa Iramba mkoani Singida, uliofanyika leo, tarehe 10 Septemba 2025, Rais Dkt. Samia amesema ili nchi yetu iendelee kukua kwa nyanja zote, kila Mtanzania anatakiwa kuendelea kuiamini CCM, kwani chama hiki kimekuwa kikitekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa wakati na kuleta maendeleo yanayoonekana katika kila sekta.
Rais Dkt. Samia aliwahi kutoa rai kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kumpigia kura Chama Cha Mapinduzi:
"Rai yangu kwenu, jitokezeni kuichagua CCM, wingi huu tunaouona kwenye uwanja ndio wingi huu unaotarajiwa kuja kwenye sanduku la kura."
"Haitapendeza kuona nyomi hili hapa uwanjani halafu msione kwenye masanduku ya kura."
Baada ya mkutano huo, Rais Dkt. Samia amekamilisha ratiba yake ndani ya mkoa wa Singida na sasa ataelekea mkoa wa Tabora kuendelea na ziara yake ya kampeni.
#SafariYaCCM
#SafariYaUshindi
#OktobaTunatiki✅
#KaziNaUtuTunasongaMbele
0 Comments