Tarehe: 09 Septemba 2025
Mkuranga, Tanzania
Safari ndefu na yenye matumaini makubwa ilifanywa na mgombea wa Ubunge wa Mkuranga, ndugu Abdallah Ulega, alipokuwa akitembelea vijiji, vitongoji, na kila kona ya kata ya Vikindu.
Mgombea Ulega, akiambatana na mgombea wa udiwani wa kata hiyo, aliweza kutembelea wananchi wa Vikindu na kushirikiana na makundi yote, ikiwemo mama lishe, wafanya biashara wadogo, na maafisa wa usafirishaji, ili kusikiliza changamoto zao na kueleza mikakati ya maendeleo.
Maboresho Makubwa ya Sekta Zote
Mgombea Ulega aliwahakikishia wananchi kuwa sekta zote zimepata maendeleo makubwa chini ya CCM, ikiwemo:
Elimu: Ujenzi wa shule mpya na uboreshaji wa madarasa ili kutatua changamoto kubwa ya elimu.
Afya: Upanuzi na ujenzi wa vituo vya afya na zahanati katika vijiji mbalimbali.
Maji na Umeme: Upatikanaji wa huduma hizi umekuwa tatizo la historia limepunguzwa.
Barabara: Utekelezaji wa mpango mkubwa wa mtandao wa barabara unaounganisha vijiji na vitongoji.
Mgombea Ulega aliwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya Kata ya Vikindu.
0 Comments