DK.MWINYI AIOMBA AZAM KUPELEKA BOTI PEMBA, SERIKALI KUJENGA GATI YA KISASA MARUHUBI

 


NA MWANDISHI WETU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema usafiri wa baharini ni muhimu katika nchi kama Zanzibar, na Serikali inafanya juhudi za kuimarisha miundombinu na mazingira ya huduma za usafiri wa baharini. 

Aliwashukuru wawekezaji wa Azam Marine kwa kuleta vyombo vya usafiri wa baharini vyenye ubora, na kueleza kuwa mchango wao ni muhimu katika kurahisisha huduma za usafiri wa baharini. 

Aliongeza na kusema; ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma una umuhimu katika kukuza uchumi na kuimarisha huduma za jamii ikiwa ndio malengo ya Serikali.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo wakati wa uzunduzi wa boti mpya Kilimanjaro VIII ilizinduliwa rasmi leo tarehe: 24 Aprili, 2023 Hoteli ya Verde, Mtoni.

Aidha  Rais Dk.Mwinyi amesema malengo ya Serikali ni kuzipatia ufumbuzi wa muda mrefu changamoto zitokanazo na msongamano wa abiria , ufinyu wa nafasi wa bandari kuu ya Malindi kwa kutekeleza mradi wa  ujenzi  kisasa wa Ferry Terminal eneo la Maruhubi  kwa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi. 

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi amewaomba kampuni ya Azam Marine kufanya safari   kati ya Unguja na Pemba ikiwezekana na Tanga katika kuwarahisishia wananchi huduma za usafiri. 

Post a Comment

0 Comments