SERIKALI YAUNGANISHA MIFUMO YA KIELEKTONIKI YA UTOAJI LESENI KATIKA SEKTA YA UTALII

 


NA MWANDISHI WETU

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema  imeunganisha mifumo ya utoaji leseni katika Sekta ya Utalii kupitia mfumo wa kieletroniki wa MNRT – Portal kwa lengo la kuongeza tija katika utoaji wa huduma na kurahisisha mchakato wa utoaji wa leseni za biashara za utalii.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema hayo leo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Cecilia Paresso aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuunganisha mifumo ya utoaji wa leseni katika sekta ya utalii ili kurahisisha upatikanaji wa leseni.

Ameongeza kuwa hatua hiyo imepunguza gharama, muda na kuongeza wigo wa ushiriki wa wananchi na wawekezaji mbalimbali katika biashara za utalii.

Aidha, kuhusu uhai wa leseni ya biashara za utalii kuendana na kalenda ya Serikali, Mhe. Masanja amefafanua kuwa Serikali imeshaanza kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali hususan wadau wa masuala ya utalii kuangalia endapo  kanuni za leseni hizo zikipitiwa upya zitaleta tija katika utoaji wa leseni.

Post a Comment

0 Comments