RC KUNENGE AWATAKA WATANZANIA KUJIVUNIA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

 


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akifungua kongamano la miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani humo.





Matukio mbalimbali katika picha kwenye kongamano la miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika Kibaha Mkoani Pwani.

NA MWANDISHI WETU, PWANI

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, amewataka Watanzania kujivunia muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kunenge ametoa Kauli hiyo leo Aprili 24, 2023 Mkoani Pwani akifunguka kongamano la miaka 59 ya Muungano huo lililofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere.

Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kwamba yapo mataifa mengi na makubwa ambayo yameshindwa kudumisha Muungano wao lakini Muungano huu umedumu na kuwa wa mfano.

“Ni jambo la kujivunia hadi sasa kuwa na Muungano huu, mataifa mengi na makubwa yameshindwa kuungana,” amesema RC Kunenge na kuongeza,

“Hivyo tunajivunia kuwa na Muungano huu, kwani ni Muungano wa kihistoria, tumeona mataifa mengine yakitumia njian nyingine za kuungana ikiwemo kuanzia kiuchumi na kadhalika,”.

RC Kunenge ametumia fursa hiyo kuongeza Awamu zote za Serikali zilizopita kwa kuulinda na kuudumisha Muungano huu hususan kipindi hiki cha utawala wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua katika kutatua kero za Muungano.

Kadhalika Kunenge amesema ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha analinda na kuutunza Muungano huu.




Post a Comment

0 Comments