Zanzibar:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania inajivunia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kama mfano barani Afrika.
Ameyasema hayo leo tarehe 25 Aprili alipohutubia Kongamano la Miaka 59 kuadhimisha Muungano wa Tanzania lililofanyika ukumbi wa Idris Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amewashukuru watoa mada wa Kongamano hilo, Profesa Patrick Loch Otieno Lumumba kutoka Kenya kwa mada ya umuhimu wa Muungano na umoja katika bara la Afrika na Waziri mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Stephen Wassira kwa kuwasilisha mada ya historia ya umuhimu wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Mhe.Balozi Mohamed Hamza mada yake ikijikita katika fursa zilizopo kwa vijana ndani ya Muungano.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema kuwepo kwa amani kwa taifa ni faida mojawapo ya Muungano kwa maendeleo alibainisha kuwa awamu zote zilizopita za utawala mpaka sasa zimekuwa zikidumisha uhusiano mwema, utamaduni, lugha fursa nyingi za ajira ushiriki wa siasa na kutumia rasimali zilizopo kwa pande zote mbili za Muungano.
0 Comments