HUSNA SEKIBOKO ATOA RAI KWA WANANCHI KUENDELEA KUTUMIA NA KUIBUA BUNIFU ZA NDANI.

 


Na mwandishi wetu Dodoma 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Elimu ya Bunge, Mheshimiwa Husna Sekiboko ameyasema hayo leo tarehe 28 Aprili 2023 katika halfa ya kuhitimisha Wiki ya Ubunifu Kitaifa , Uwanja wa Jamhuri- Jijini Dodoma 

"Kwa Niaba ya Kamati ya kudumu ya Bunge na kwa Niaba ya Bunge zima la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitumie fursa hii, kwanza kuwapongeza Wizara ya Elimu kwa hatua hizi madhubuti za kuendeleza ubunifu na ugunduzi kwa niaba ya Bunge" alisema mhe. Sekiboko

" Jambo hili ni kubwa, ni jambo jema na likiwa endelevu litatufikisha katika ile Tanzania ya viwanda tunayoifikiria na tunayoiota hongereni sana, kwa niaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dkt. Tulia Ackson pokeeni hongera zenu" alisisitiza Mhe. Husna 

Aidha, Mhe Husna alitoa ombi kwa viongozi wa Wizara ya Elimu na waratibu wa Wiki ya Ubunifu Kitaifa kuona namna bora ya ku 

" Vipaji vinaokena tangu mtoto akiwa mdogo, tuisaidie Wizara ya Elimu kungundua vipaji kwenye mashule , vyuo vikuu na Taasisi mbalimbali hii itasaidia sana kwasababu inafahamika kwamba ugunduzi na ubunifu ndio chachu na chagizi ya maendeleo ya nchi " alisisitiza. 

Aidha, Mhe. Sekiboko alihitimisha kwa kutoa rai kwa wanafunzi, Wajasirimali na wananchi kuendelea  na utamaduni wa kutumia bunifu 

Mheshimiwa Husna alihitimsha kwa kusema kuwa jambo hili ni kubwa na tumeona likifanyika toka 2019 hapa viwanja vya Jamhuri na Siku ikiwapendeza tuleteeni kwenye maeone ya mikoani ili turned namna ya kutia fursa kwa vijana kujifunza na kuonesha bidhaa za kibunifu kwa faida ya wananchi wote. 


Post a Comment

0 Comments