SHURA YA MAIMAMU YALAANI WIZI WA MALI ZA UMMA, MMONYOKO WA MAADILI NCHINI, WAMSIHI RAIS SAMIA KUCHUKUA HATUA

 


Dar es salaam:
Shura ya maimamu Tanzania imetoa waraka wa sikukuu ya Eid ambao umelaani kuhusu mmomonyoko maadili na ubadhirifu wa Mali za umma kumsihi Rais Dkt Samia kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya  waliotajwa kwenye ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG.

Akisoma tamko hilo Katibu wa Shura ya maimamu Tanzania, Sheikh Ponda ISSA Ponda katika baraza la Eid lililofanyika katika msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni Jijini Dar es salaam alisema wabadhirifu wa Mali za umma ambao wamekuwa wakitajwa mara Kwa mara kwenye ripoti za CAG bila kuchukuliwa hatua zozote Hali ambayo inawapunguzia matumaini wananchi juu ya watawala wao waliowapa dhamana.

Alisema Rais Samia pamoja na hatua za awali alizochukua anapaswa kuchukua hatua kali dhidi yao kisha kuteua tume maalum na huru ya kuchunguza ubadhirifu wa Mali za umma na baadaye bunge pia lichukue hatua stahiki dhidi ya wabadhirifu hao.

Aidha Shura ya maimamu Tanzania imependekeza suala la maadili liwe ni kipimo Cha mtu kupewa uongozi ili kuondoa uwepo wa viongozi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakifuja Mali za umma.

“Kwa kweli hatuoni kama nchi yetu Ina tatizo la fedha au rasilimali hapana, lakini inaonekana nchi ina tatizo la watu kutokuwa na maadili ambapo mporomoko wa maadili ni mkubwa Kwa kiwango ambacho imekuwa sasa ni ugonjwa wa watanzania wengi hasa viongozi, na tumeona pia Rais ameshachukua hatua mbalimbali na sisi kama maimamu tunaimiza Rais azidi kuchukua hatua ukiachana na zile ambazo zinasubiri mchakato wa Kibunge” Aliisema Sheikh Ponda.

Waraka huo pia umeelezea juu ya suala la mporomoko wa maadili kama chanzo kinakopelekea kushamili kwa vitendo vya ushoga na usagaji imefika wakati Kwa vyombo vya ulinzi na usalama waelimishwe ukubwa wa madhara ya ushoga kama ambavyo wanaelimishwa Kuhusu madawa ya kulevya kwani vitendo hivyo ni hatari mustakabali wa Taifa.

Aliongeza kuwa ili kutokomeza vitendo hivyo serikali kupitia wizara ya elimu inabidi ilifanye Somo la dini kama kuwa la lazima Kwa wanafunzi wote na lifanyiwe mitihani ya NECTA Kwa ngazi zote za elimu na liwe ni sehemu ya tahsusi ‘Combination’ ambazo zinahusisha masomo ya dini.

Aliongeza hatua hiyo itajenga Taifa bora na lenye maadili Kwa kumjua Mwenyezi Mungu Hali ambayo itapunguza vitendo vya mmomonyoko wa maadili na ubadhirifu wa Mali za umma ambao hutokana na watu kutokuwa na maadili mema.

katika hatua nyingine shura ya maimamu Tanzania imeiomba serikali kufuta tamko lake la mwaka 2018 kupitia barua ambayo inasemekana kuunga mkono baadhi ya vitendo vya mmomonyoko wa maadili vinavyoletwa na mataifa ya magharibi ili kuviharibu vizazi barani Afrika.

Post a Comment

0 Comments