USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA SIASA WAPIGA HATUA MWAKA HADI MWAKA

 


Msajili wa vyama vya siasa nchni Jaji Francis Mutungi akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha ya kupitia ripoti ya uchambuzi wa mapengo ya kijinsia katika nyaraka za kisera za vyama vya siasa  hapa nchini leo Aprili 25 Jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF na Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha ya kupitia ripoti ya uchambuzi wa mapengo ya kijinsia katika nyaraka za kisera za vyama vya siasa hapa nchini leo Aprili 25 Jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi amesema ushiriki wa wanawake katika siasa umekua ukipiga hatua mwaka hadi mwaka licha ya uchache wa nafasi za wanawake katika ngazi ya kutoa maamuzi na kwenye michakato ya kisiasa hivyo amevitaka vyama vya siasa kuziba mapungufu yaliyopo kwa kuzingatia usawa wa kijinsia katika vyama vyao.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Aprili 25 Jijini Dar es Salaam  wakati wa uzinduzi wa warsha ya kupitia ripoti ya uchambuzi wa mapengo ya kijinsia katika nyaraka za kisera za vyama vya siasa ambapo alibanisha kuwa wanawake wana nafasi  ya kushiriki katika nafasi za kutoa maamuzi na kukuza Demokrasia hapa nchini.

Jaji Mutungi amesema kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika vyama vya siasa na maendeleo ya Demokrasia kutokana na wingi wao hivyo kuna haja ya kuwa  na uwiano sawa wa nafasi za uongozi unaozingatia jinsia.

Aidha Jaji Mutungi amewataka wanawake kuwa na umoja na kuacha misuguano ya kisiasa wao kwa wao kwani hurudisha nyuma maendeleo ya ushiriki wa wanawake katika siasa.

kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF na Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba amesema mkutano huo umelenga kuangazia ushiriki wa wananawake katika kujenga mfumo wa demokrasia hapa nchini.




Post a Comment

0 Comments