Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI), Dokta. Revocates Mushumbusi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali kujadiliana juu ya namna bora ya uokoaji wa asili jijini Dar es salaam.
Mhifadhi Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu nchini Bwana Juma Mwangi akifafanua jambo wakati aliongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali kujadiliana juu ya namna bora ya uokoaji wa asili jijini Dar es salaam
Dar es Salam:
Mikoa ya Shinyanga, Singida na mingine yenye asili ya kame na Tabia ya nchi imetajwa kuwa kinara wa uharibifu mkubwa wa mazingira nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau kutoka taasisi mbalimbali za misitu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI), Dokta. Revocates Mushumbusi amesema lengo la warsha hiyo ni kujadiliana juu ya uokoaji wa asili.
“Uharibifu wa mazingira ni mkubwa sana unasababishwa na matumizi ya binadamu ikiwemo kilimo cha kuhamahama, ufugaji, vyanzo vya maji na kushindwa kufuata utaratibu wa mipango miji,”. Alisema Dk. Mushumbusi.
Dk. Mushumbusi alibainisha kuwa katika kikao cha nchi 32 za bara la Afrika kilizokaa mwaka 2018 kwa lengo kujadiliana namna ya kurejesha hekta milioni mia moja za uoto wa asili ifakapo 2030.
"Kikao hiki utekelezaji wa mkakati wa nchi za Afrika ambazo Tanzania ni miongoni mwao zilizokaa na kukubaliana kurejesha hekta milioni tano za uoto wa asili ifikapo mwaka 2030,” Alisema Dk.Mushumbusi.
Dk. Mushumbusi aliongeza kuwa kikao hiki cha leo ni kutimiza ahadi malengo makubwa waliyonayo ya kuhakikisha kuwa nchi zote zinaendelea kutoa elimu ya jinsi ya kurejesha uoto wa asili.
Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu nchini Bwana Juma Mwangi amesema kwa mujibu wa ripoti zilizopo jumla ya Hekta 469,000 huaribiwa kila mwaka kutokana na kuanzisha makazi holela na mengineyo.
“Kupitia mkutano huu wadau wataweza kufungua fursa mbalimbali kwao na kusaidia uongoaji wa ardhi iliyoharibika na kuhakikisha ardhi inarudi kama ilivyokuwa,” Alisema Bw. Mwangi.
Naye Mkurugenzi wa Miradi Kisiki Hai, Njamasi Chiwanga amesema Taasisi yake imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa kukusanya nguvu kutoa elimu kwa jamii hususani vijijini ili kufikia malengo hayo.
“Taasisi yetu zaidi ya asilimia 55 tunafanya kazi hivyo zaidi ya Vijiji mia nne misitu iko chini yao tuna mikakati mingi ya kurejesha ardhi na uoto wa asili,” amesema Chiwanga
0 Comments