Na WAF-DODOMA
NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amebainisha kuwa, Wizara inakamilisha mapitio ya miundo ya kada za afya ambayo inatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2023 na kuwasilishwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala na Bora kwa ajili ya kupata idhini ili watumishi waanze kunufaika kutokana na maboresho hayo.
Dkt. Mollel amesema hayo leo Aprili 28, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Dkt. Alice Kaijage katika Mkutano wa kumi na moja kikao cha 15 Jijini Dodoma.
"Wizara inakamilisha Mapitio ya Miundo ya kada za afya ambayo inatarajiwa kukamilika Mwezi Mei 2023 na kuwasilishwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala na Bora kwa ajili ya kupata idhini." Amesema Dkt. Mollel
Ameendelea kusema kusisitiza kuwa, kukamilika kwa maboresho ya miundo hii kutasaidia kukidhi mahitaji ya kiutumishi kwa wataalamu mbalimbali wa afya wakiwemo Madaktari Bingwa na Wataalamu wengine waliopata fursa ya kujiendeleza katika kada zao.
Aidha, Dkt. Mollel amesema, kwa sasa Serikali inatekeleza Waraka wa Maendeleo ya Utumishi namba 1 wa mwaka 2009 kwa kada zilizo chini Wizara ya Afya ambao umeainisha miundo na sifa za wataalamu mbalimbali wanaopaswa kuajiriwa na kufanya kazi katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini.
0 Comments