PWAGI WAPONGEZWA KWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KWA NGUVU ZA WANANCHI

 


Na mwandishi wetu


Serikali imewapongeza wananchi wa kata ya Pagwi jimbo la Kilindi mkoa wa Tanga kwa juhudi za ujenzi wa kituo cha Afya kwa kutumia nguvu zao wenyewe ikiwa ni sera ya mpango wa maendeleo ya Afya ya msingi kwa wananchi kushiriki na semrikali kuunga mkono.

Pongezi hizo za serikali zimetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange kwa niaba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengera bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Lulenge aliyetaka kujua mpango wa serikali kupeleka fedha Mil. 100 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha Afya.

Akijibu swali hilo kwa kuunga mkono juhudu za wananchi Mhe. Dkt. Dugange amesema “serikali inatambua umuhimu wa kupeleka fedha hii haraka iwezekanavyo na hii bajeti ya 2024/25 ni ‘tentatively’ lakini tuna uwezo wa kutafuta fedha kupitia kwa wadau mbalimbali na kuona namna nzuri ya kwenda kukamilisha kituo hiki mapema zaidi” amesema

Post a Comment

0 Comments