TRUMP AMEMTEUA MENEJA WAKE WA KAMPENI KUWA MKUU WA UTUMISHI IKULU

 



Na mwandishi wetu

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amefanya uteuzi wa kwanza wa Wasaidizi wake wakati anajiandaa kuchukua madaraka rasmi mwezi January mwakani 2025 baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika November 05,2024.

Trump amemteua Meneja wake wa kampeni Susie Wiles kuwa Mkuu wa Utumishi wa Ikulu ya White House/ Mtendaji Mkuu wa Ikulu, wadhifa wenye jukumu la kusimamia shughuli za kila siku za ofisi ya Rais na Watumishi wake ambapo Susie anakuwa Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo Nchini humo.

Susie atakuwa na jukumu pia la kuwaajiri Wafanyakazi wa Rais na  kuwaongoza Watumishi kupitia Ofisi ya Rais na kusimamia shughuli zote za kila siku za Wafanyakazi, pia atakuwa Mshauri wa Rais Trump kuhusu masuala ya sera na ataongoza na kusimamia maendeleo ya sera.

Kwenye taarifa yake, Trump amesema Susie amemsadia kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi uliomalizika na alikuwa na mchango mkubwa kwenye kampeni zake za mwaka 2016 na 2020, Trump amemwelezea Susie kuwa Kiongozi madhubuti mwenye maarifa na Mbunifu.




Post a Comment

0 Comments