Na mwandishi wetu, Morogoro
Shirika la umeme Tanzania ( TANESCO ) limetwaa tuzo ya mshindi wa kwanza ya uzalishaji umeme na usambazaji, zilitolewa mkoani Morogoro kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi.
Tuzo hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako iliyokwenda sanjari na Maonesho ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi za umma na binafsi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo Afisa Mwandamizi Afya na usalama mahala pa kazi Nelson Mnyanyi amesema TANESCO inazingatia, inatekeleza pamoja na kishi kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Mazingira salama na afya ni kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.” Kwa kutimiza sheria ya usalama mahala pa kazi ya mwaka 2003.
“Kupitia sheria ya usalama mahala pa kazi ya mwaka 2003, tumeyengeneza sheria na sera ya afya mahala pa kazi ya TANESCO ambayo kimsingi ni sera mpya ambayo inasimamiwa na utawala ili kuzingatia usalama na afya mahala pa kazi.” Alisema.
Pia amesema TANESCO inakanuni mbalimbali ambazo inawasisitiza wafanyakazi wao kufuata taratibu zote za afya na usalama mahali pa kazi ili kupunguza ajili wawapo kazini.
“TANESCO suala la mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi ni kipaumbele chetu, ukiangalia hata hapa kwenye banda letu, utaona hata viti wanavyotumia watumishi wetu ni vile vinavyotakiwa kwa mujibu wa OSH.” Alisema Mnyanyi
Akihutubia katika kilelecha hafla hiyo, Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kusimamia masuala ya usalama na afya mahala pa kazi kwa kuwa ni haki ya msingi ya kila mfanyakazi nchini.
Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine duniani kuiadhimisha siku hii, lengo kubwa ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu sehemu za kazi
0 Comments