TASAC YAWATAKA WAMILIKI NA WASAFIRISHAJI WA MAJINI KUZINGATIA KANUNI NA MASHARTI YANAYOTOLEWA NA MDHIBITI

 



Na mwandishi wetu Morogoro

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limewataka wasafirishaji wa majini kuzingatia usalama na afya mahala pa kazi ili kuepuka ajali wawapo kazini pamoja na kutunza mazingira ya bahari na maziwa.

Afisa  Uhusiano Mwandamizi wa TASAC Amina Miruko akizungumza Mjini Morogoro kwenye maonyesho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi amesema katika kuhakikisha usalama wa vyombo vya usafiri vya majini vinakuwa salama ni vyema wamiliki na wasafirishaji kuzingatia kanuni na masharti yanayotolewa na wadhibiti.

Amesema moja ya kazi zao ni kukagua meli za kigeni zinazotia nanga katika bandari zote nchini, kudhibiti na kuidhinisha vifaa vya huduma vya usalama majini vinavyotumiwa na watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC.

Pia kusimamia na kufuatilia mienendo na tabia za watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC na kutafuta ufumbuzi wa malalamiko na migogoro kati ya watoa huduma , watumiaji wa huduma pamoja na kutoa elimu kwa umma.

Kwa upande wake Afisa Msajili wa vyombo vya majini Sweet Christopher amesema moja ya majukumu ya TASAC yalioanishwa kwenye sheria ya uwakala wa meli Tanzania sura 415 kifungu cha 7, 11 na 12 ni kukagua vyombo vya usafiri majini vikiwemo Boti, Mitumbwi na Meli kubwa zinazosajiliwa Tanzania Bara.

Amesema shirika limeweka taratibu ya kutoa elimu kwa wamiliki  pamoja na watumiaji wa vyombo vya majini hasa wavuvi kwenye mialo yote hapa nchini lengo likiwa ni kupunguza ajali za majini .
“Kila mwaka shirika linatoa elimu kupitia njia mbalimbali, hata hapa kwenye banda letu ukiangalia tuna majaketi ya kujiokoa na vifaa vinginevya usalama. ” alisema


“Pia tuna utaratibu wa kukutana na wavuvi katika mikoa mbalimbali hapa chini hasa kwenye maziwa na bahari pia  tumekuwa tukitoa elimu kwenye mialo ya Dar Es salaam, Mwanza, Tanga, Kagera na maeneo yote yenye mialo.” Aliongeza.

TASAC ni shirika la umma lililochini ya Wazara ya ujenzi na uchukuzi lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya wakala wa meli Tanzania sura 415 .


Naibu waziri, ofisi ya waziri mkuu - kazi, vijana, ajira na wenye enye ulemavu Patrobas Katambi Akipokea zawadi kutoka kwa Afisa uhusiano Mwandamizi TASAC Amina Miruko  kwenye maonyesho ya maadhimisho ya siku ya kitaifa ya usalama mahala pa kazi yaliofanyika Mjini Morogoro






Post a Comment

0 Comments