WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAMEFARIKI BAADA YA KUVUTA HEWA CHAFU YA MOSHI WAKIWA WAMELALA

 


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro.


NA MWANDISHI WETU 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la vifo vya watu wanne wa familia moja ambao wamepoteza maisha baada ya kuvuta hewa chafu ya moshi kutoka kwenye jenereta walilowasha ndani ya nyumba na baadae kulala, tukio hilo lililotokea tarehe 19. 04. 2023 maeneo ya Chang’ombe, Temeke, Jijini Dar es salaam.


Taarifa zilieleza kuwa tarehe 18. 04. 2023 majira ya saa 4 :00 usiku watu hao waliwasha jenereta baada ya umeme kuzimika na kuliweka ndani ya nyumba. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa watu hao walipoteza maisha baada ya kuvuta hewa inayodaiwa kuwa ni hewa chafu ya moshi iliyokuwa inatoka kwenye jenereta baada ya kuwashwa.

Waliopoteza maisha ni Kazija Mohamed (21), Munir Ibrahim (7), Munira Ibrahim (6) Muyyat Ibrahim (3). Mume na mke ambao ni Ibrahim Juma (28) na Aisha Ayubu (29) wote wakazi wa Kilimahewa, Chang’ombe hali zao sio nzuri an wanenedelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kwa kushirikiana na mamlaka zingine.

 

Muliro J. MULIRO - SACP

Kamanda wa Polisi


Post a Comment

0 Comments