KONDOA WATAKIWA KUMALIZA UJENZI JUNI 15,2023

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu akikagua ujenzi wa jengo la wazazi linalojengwa katika Hospitali ya Mji Kondoa ambaloliko katika hatua za umaliziaji. Ujenzi huo unaenda sambamba na majengo mengine mawili ya upasuaji na chumba cha kuhifadhi maiti. Serikali imetoa kiasi cha Shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali kongwe nchini.

Na mwandishi wetu 

Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 900,000,000 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Mji wa Kondoa ili kuboresha utoaji wa huduma za afya.

Haya yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mji Kondoa Bw. Paul Sweya wakati akisoma taarifa ya hatua za ujenzi na ukarabati wa majengo matatu mbele ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu ambae yuko kwenye ziara ya kukagua utekezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Kondoa.

Bw. Sweya emesema  kiasi hicho cha fedha kimetumika kujenga majengo matatu ambayo ni Jengo la wazazi, Jengo la upasuaji na Jengo la kuhifadhia maiti ambayo  ujenzi wake unaendelea.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amesema ni vema ujenzi wa miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kuelekeza kuwa kufikia tarehe  15 Juni, 2023 ujenzi uwe umekamilika.

"Ndugu zangu hatutaki kabisa kuvuka mwaka na miradi viporo, hivyo nitarudi tena hapa tarehe 15 Juni 2023 kama tulivyokubaliana ili majengo haya yawe yamekamilika” Gugu amesisitiza.

Pia, amewataka kutumia kiasi cha fedha hizo kwa ajili ya ukarabati wa wodi ya Watoto na kujenga njia za kutembelea kwa ajili ya kuunganisha jengo moja na lingine.

Halmashauri ya Mji wa Kondoa inaendelea na utekelezaji wa miradi mingine ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Kituo cha Afya Serya unaogharimu milioni 500,000,000 fedha za tozo kutoka Serikali Kuu. Fedha hizi ni kwa ajili ya ujenzi wa Maabara, Jengo la Mapokezi ya Wagonjwa wa nje, Jengo la Upasuaji na Jengo la Wazazi pamoja na Zahanati ya Ausia na Chandimo ambazo gharama yake ni milioni 134,000,000 na ujenzi uko katika hatua mbalimbali.

Ziara ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu inaendelea siku ya pili kwa kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.  Gugu akipata maelezo kutoka Mwalimu Anthony Dihemba wa Shule ya Sekondari Bicha kuhusu vyumba viwili vya maabara vilivyokamika na kugharimu kiasi cha shilingi Milioni 30

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bicha iliyopo katika Halmashauri ya Kondoa Mji. Pamoja na mambo mengine Gugu amewasisitiza kusoma kwa bidii na kutunza miundombinu inayojengwa na Serikali ikiwa ni pamoja na madarasa na maabara.

Post a Comment

0 Comments