MISS DARZONE WAINGIA KAMBINI JIJINI DAR

Nasra Swalehe Mrembo anaeshikilia taji la Miss Darzone 2022 akizungumza machache mara baada ya warembo wa shindano hilo kuingia kambini kwa siku 13 ambapo fainali ya shindano hilo linatarajiwa Mei 13,2023 katika ukumbi wa superdome Masaki Jijini Dar es salaam

NA MWANDISHI WETU 

WAREMBO  13 wa Shindano la Miss Dar zone waingia kambini rasmi Jijini Dar es salaam  huku wakihaidi mengi mazuri ambayo yatakuwa mfano wa kuigwa kwa warembo wengine.
 

Akizungumza na Wanahabari Leo Mei mosi Mratibu wa shindano hilo Linda Samson amesema mchakato wa sasa ni warembo hao kuingia kambi na kufatiwa na ratiba ya kutembelea mbuga za Wanyama Mkoani Tanga.
 

"Tayari warembo wetu wanaingia kambini Royal hoteli Jijini Dar es salaam  watakaa kambini kwa siku 13 hadi kufikia kilele cha Shindano hili."

Pia amesema tayari wamepata mualiko kutoka bungeni Dodoma kwa ajili ya kukutana na viongozi mbalimbali na kutoa mualiko rasmi wa kushiriki katika Fainali ya shindano hilo.


Hata hivyo amesema warembo hao kuwasili kambini ni kiashiria tosha kuwa Shindano hilo linaenda kukamilika kwa asilimia 100 kutokana na muitikio huo wa warembo wenyewe.


Pia amesema Shindano hilo linatarajiwa kufika tamati mei 13,2023 katika ukumbi wa superdome Masaki huku akisemq kwa sasa zawadi ya Mshindi itawekwa hadharani mapema kabla ya siku ya tukio.


Kwa upande wake Mrembo anaeshikilia taji hilo la Miss Darzone  2022 Nasra Swalehe amesema Warembo wa Mwaka huu wote wazuri lakini mmoja wao ndio atakaeweza kupokea taji hilo Usiku wa Mei 13,2023.


Aidha,amewaasa warembo kutumia vizuri jukwaa hilo la urembo kwa maslahi ya kusaidia jamii zao.


"Nimepata faida nyingi kupitia jukwaa la Miss Darzone lakini nidhamu imeniwezesha kufika mbali zaidi na kuaminika katika jamii  kuwa urembo sio uhuni."


 

Post a Comment

0 Comments