Na mwandishi wetu
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na Iringa MotorSports Club wameandaa mbio za magari "CMC Automobile Southern Forest Rally " zinazotarajiwa kufanyika Mei 14 mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Afisa Utangazaji utalii ikolojia kutoka TFS Anna Lauwo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Amesema hiyo ni sehemu ya kutangaza na kuhamisha utalii ikolojia pamoja na kuendeleza Mashindano ya magari nchini.
Amesema CMC Automobile ni zao jipya la mbio za magari ndani ya msitu,pia Mashindano hayo yatazinduliwa rasmi tarehe 13/05/2023 Iringa mjini na Mashindano kuanza tarehe 14/05/2023 katika misitu.
Tunayo mashamba takribani 24 ya misitu ambayo yanafaa kwa mbio za magari,waendesha baiskeli,mbio za miguu,mbio za pikipiki, kwahiyo tunawakaribisha watu mbalimbali ambao wanaanda matukio kama haya ili waweze kuandaa katika hayo mashamba yetu" Amesema Anna.
Pia ameongeza kuwa katika mashamba hayo ya misitu kuna fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo ujenzi wa hotel,migahawa na kambi hivyo TFS inawakaribisha wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika maeneo hayo na kutoa huduma kwa watu wanaofanya utalii katika misitu hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Iringa MotorSports club Amjad Khan ameushukuru uongozi wa TFS kwa ushirikiano wao na kuwapatia maeneo salama na yenye hadhi kwa kufanyia mbio hizo na ni nafasi ya kipekee ya kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja yani mbio za magari na kutangaza utalii.
Aidha amebainisha kuwa Mashindano hayo yatakuwa na washiriki kutoka katika maeneo mbalimbali ikiwemo wa hapa nchini,pia kutoka uganda na kenya,urefu wa Mashindano hayo ni Kilometer 20 mpaka 26 na zitakuwa zinarudiwa.
"Mashindano haya ni fursa ya kipekee ya kuwakutanisha wadau wote kwasababu kwenye mchezo huo pia wapo wapenzi wengi sana,mashabiki wengi sana ambao wanapenda kushiriki mchezo huo kwahiyo kupitia mbio za magari tumeona mwitikio ni mkubwa na imetusaidia sisi pia kupata wageni kutoka sehemu mbalimbali"
" Tukiangalia mchezo wetu huu tunaotarajia kuufanya tarehe 13 wengi wao wanakuja kwa mara ya kwanza kutoka nchi mbalimbali just kuja ku-experience lile shamba letu la Southern ambalo kwao ni kitu kigeni" Alisema Khan.
0 Comments