Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mradi wa nyumba za mkazi wa Magomeni (Watumishi House).
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema wanajaribu kuona sababu ya kuiongezea bajeti Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) ili iweze kujenga majengo mengi zaidi hapa nchini.
Aidha, amesema taasisi hiyo changamoto kubwa iliyokuwa nayo ni mtaji mdogo, kwa hiyo ikisaidiwa itafika mbali zaidi kutokana na kasi iliyokuwa nayo kwa sababu ndani ya muda mchache imejenga nyumba zaidi ya 900.
Waziri Simbachawene amesema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, baada kukagua Mradi wa Nyumba za Makazi Magomeni (Watumishi House), ikiwa ni moja ya ziara zake za kikazi katika wizara hiyo.
"Tunajaribu kuona sababu ya kuwaongezea bajeti kwa ajili ya maendeleo ili kusaidia iweze kwenda maeneo mengi zaidi, kwa sababu mtumishi akiishi katika makazi bora na yaliyojirani anapofanyia kazi inamsaidia na kumfanya awe na ufanisi,"
"Kwa hiyo ni adhima ya Serikali ni kuhakikisha kwamba inaisadia Watumishi Housing, lakini tunaamini kabisa kwamba kama wakisaidiwa na kupewa nguvu kubwa zaidi wanauwezo wa kufika kila mahali," alisema Simbachawene
"Kutokana na ubunifu waliyoufanya wameanzisha kitu kinachoitwa mfuko wa Faida Fundi, umekuwa kwa kasi kubwa na sasa umefikia mtaji wa karibu Sh bilioni 12.7 na umeweza kufikia thamani karibu Sh bilioni 15 na hii yote ni katika kujenga nguvu ya watumishi housing katika kutekeleza jukumu lake, "
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa WHI, Dkt. Fred Msemwa amesema kupitia juhudi zinazochukuliwa na serikali na zile zinazofanywa na menejimenti tutaweza kufikia lengo la kuwa na mtaji mzuri ili waweze kujenga nyumba nyingi zaidi.
Amesema mfuko huo ulianza mwaka huu, mwezi Januari na ambapo kwa sasa umefikisha takribani sh bilioni 15 na thamani ya vipande imeongezeka kutoka Sh 100 za wakati huo hadi Sh 103.42 kwa hiyo ni ukuaji mzuri, ambapo kwa mwaka wanaweza tukafikia ukuaji wa asilimia 10 hadi 11.
"Ilikukabiliana na uhaba wa viwanja, tumekuwa tukishirikiana na halmashauri za miji pamoja na manispaa ambazo kimsingi ndiyo wanaomiliki maeneo kwa hiyo wamekuwa wakitupa ushirikiano mzuri kututafutia maeneo kwenye wilaya zao na mikoa yao," amesema
"Kwa sasa mradi unaondelea ni mkubwa wa nyumba 1000 uliyopo jijini Dodoma, ambapo katika hizo nyumba tayari tumeshajenga nyumba 203 na zote zimeshauzwa, na katika jiji la Dar es Salaam mradi unapendelea kwa sasa ni mradi wa Kawe ambapo tunajenga nyumba 560,"amesema
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa (wa kwanza kulia) wakati akikagua Mradi wa Nyumba za Mkazi wa Magomeni (Watumishi House).
0 Comments