Na mwandishi wetu
-Asema sio tu katika nyanja ya Viwanda bali hata nyanja zingine
-Abainisha kuwa Mkoa wa Pwani una viwanda vingi lakini soko lake kubwa ni Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo Novemba 01,2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila alipotembelea Kiwanda cha Goodwill Mkuranga Pwani na kupokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge.
RC Chalamila amemshukuru Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji Goodwill muwekezaji toka China ni kielelezo cha juhudi kubwa za Serikali kuvutia uwekezaji Nchini
Aidha RC Chalamila amesema Mkoa wa Pwani una viwanda vingi na wawekezaji wanaendelea kuja kuwekeza ambapo Soko kubwa ni Dar es Salaam hivyo Mkoa utaendelea kushirikiana na Pwani sio tu katika Viwanda bali hata katika nyanja zingine kwa masilahi mapana ya wananchi wa pande zote mbili.
Sanjari na hilo amepongeza kiwanda cha Goodwill kwa kutoa fursa za ajira kwa wazawa, ambapo ametoa rai kwa kiwanda hicho ambacho kinazalisha tiles kuendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora pamoja na kurejesha sehemu ya faida kwa jamii (CSR)
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge amesema pwani itaendelea kusimamia maono ya Mhe Rais kwa kuhakikisha inavutia wawekezaji kwa kuwa uwekezaji huo unafaida kubwa ya kiuchumi lakini pia unatupa heshima ndani na nje ya Tanzania kwa kuwa bidhaa zinazotengenezwa zinakuwa zinaonyesha zinatengenezwa Tanzania-(Made in Tanzania)
0 Comments