Mratibu wa Mafunzo ya Vijana wa Mafunzo ya Utawala wa Internet kwa nchi 16 zilizo Kusini Mwa Afrika na Rais Internet Society Tanzania Nazar Kirama akizungumza katika mafunzo hayo jijini Dar es Salaam.
Na mwandishi wetu
Vijana wametakiwa kutumia Internet katika katika kujiletea maendeleo kutokana kuwa Dunia kuwa kijiji kwa kuhisisha mtu moja ndani nchi kujadili fursa na mwingine nje ya nchi kufanya kutengeneza biashara.
Hayo ameyasema Mratibu na Rais wa Internet Society Tanzania Nazar Kirama wakati wa wa mafunzo ya Vijana wa Kusini Mwa Afrika kwa njia ya Mtandao na Uso kwa Uso na baadhi ya vijana katika katika jiji la Dar es Salaam.
Amesema kuwa wanafundisha vijana wa nchi 16 Kusini Mwa Afrika juu ya utawala Internet kutokana na Internet kuwa haina mtu mmoja hivyo inahitaji kila mmoja kufundishwa.
Kirama amesema kuwa vijana wakiwa na uelewa Internet namna bora ya kuitumia itaondoa mambo yasiyo ya msingi na badala yake itachochea maendeleo ya mtu mmoja moja.
Amesema kuwa nchi imepiga hatua kubwa katika matumizi ya intenet hususan kwa serikali kuweka mifumo yote kwa njia ya internet iwe kwenye huduma ya kusajili pamoja na kutuma fedha za malipo ya serikali ni kwa kutumia mtandao.
Aidha amesema kuwa kwa vijana kutumia bando kwenye internet kwa mambo yasio ya msingi ni kujitafuta shimo la umasikini na kutokana mtu aliyegundua hakutaka kuwepo kwa matumuzo ya hovyo.
Amesema kuwa dunia inakwenda kasi katika matumizi ya internet hivyo kasi hiyo lazima iendane na matumizi ya kiuchumi kila mmoja.
Hata hivyo amewasaa vijana kutoweka vitu ambavyo ni kinyume cha maadili kutokana na internet haisahu kitu kilichowekwa ambapo aliyeweka atapata hasara pale anapotaka ajira kwa watu kuingia kutafuta sifa binafsi ambazo zitapatikana katika mtandao.
Kirama amesema katika vijana katika Teknolojia ni fursa ya kutumia internet kufanya mambo mengi ya ubunifu na yote yanapatikana kwenye matumizi ya Internet.
Mratibu wa Mafunzo ya Vijana wa Mafunzo ya Utawala wa Internet kwa nchi 16 zilizo Kusini Mwa Afrika na Rais Internet Society Tanzania Nazar Kirama akiendesha mafunzo kwa njia ya Mtandao kwa nchi 16 akiwa Jijini Dar es Salaam.
Abeid Bushira wa UMUKA HUB Akizungumza kuhusiana na mafunzo walioyapata katika kwenda kutoa elimu kupitia taasisi yao, jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa chuo Apple Valley Insititute of Health and Science Monica Shimo akizungumza kuhusiana na matumizi mabaya ya internet baada ya kupata mafunzo , jijini Dar es Salaam.
0 Comments