KATIBU MKUU ABDULLA AZINDUA KITABU CHA KLABU ZA KIDIGITI, ATOA WITO KWA WALIMU WAKUU

 


Na mwandishi wetu 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla amezindua kitabu cha kuanzisha na kuratibu Klabu za Kidigiti.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Novemba 2, 2023 jijini Dar es Salaam Abdulla ametoa wito kwa wakuu wa shule za Serikali, binafsi na vyuo kuhamasika kuanzisha Klabu hizi za Kidigiti.

“Leo tunaandika historia kwa kuzindua Kitabu cha kuanzisha na kuratibu Klabu za Kidigiti. Nitoe wito kwa walimu wakuu wa shule za Serikali na binafsi, wahamasike kuanzisha Klabu hizi za Kidigiti, kwa kuhakikisha wanazisimamia na kufuata maadili,” amesema Abdulla na kuongeza,

“Hatuna budi kuhakikisha tunakuwa na tabia za kibunifu kuendana na mabadiliko ya Dunia. Uwepo wa Klabu za Kidigiti itasaidia Vijana kuongeza bunifu na ujuzi,”.

Abdulla amebainisha kuwa kuzinduliwa kwa Kitabu hiki ni katika kuhakikisha wananchi, hususan Vijana wanashiriki katika uchumi wa Kidigiti.

Kwamba hiyo itawezesha Vijana kujifunza na kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya kidigitali wakiwa katika umri mdogo kwani Klabu hizi zitaanzia ngazi ya shule za awali, naingia, Sekondari na vyuo vikuu.

“Ukimpa jambo kijana, umefikia jamii yote, hivyo kwa kumfundisha masuala ya Kidigiti akiwa mdogo unampa uelewa na kumjenga kuwa mbunifu na mjasiriamali,” ameeleza Abdulla.

Abdulla ameongeza kuwa Klabu za Kidigiti zitawajengea Vijana fikra chanya zitakazowasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili pamoja na kuwasiadia katika uchumi wa Kidigitili na kupata ujuzi.

Amebainisha kuwa katika mkakati wa kidigitali wa Mwaka 2023 Serikali imeainisha kuwa inataka kuwa na jamii ya kibunifu.

Hivyo ameeleza kuwa Kitabu hicho kitakuza tamaduni ya kibunifu nchini na kujenga jamii imara ya kibunifu kwamba katika Sera hiyo Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeweka malengo ya kukuza talanta.

Hivyo Abdulla amesema ila kupata jamii yenye kushiriki uchumi wa kidigitali ni lazima kuwekwa kwa Mazingira bora ya ushiriki.

Kwa upande wake Mwenyekiti w Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA) Mhandisi Othman Khatib amesema kupitia Kitabu hicho jamii itakwenda kujua namna ya kuanzisha na kuendeleza Klabu hizi.

“Lakini pia Klabu hizi zitawezesha jamii kuweza kutatua changamoto mbalimbali.
Niombe Wadau wote kusoma na kuelewa Kitabu hiki na kwa pamoja tutaweza Kufikia uchumi wa Kidigiti," amesema Mhandisi Khatib.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari amesema kuwa Klabu za Kidigiti ni majukwaa ya hiari yanayowakutanisha wanafunzi na kuhamasishana kuhusu uelewa katika masuala ya kidigitali.

Hivyo amesema ili kuboresha uendeshaji wa Klabu hizi TCRA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Tamisemi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Maendeleo, Jinsia, Wanawake na Makundi Mwalimu wameandaa Kitabu hichokuwa mwongozo wa Masomo kwa Klabu hizo kwa ngazi ya shule za awali, msingi, Sekondari na vyuo.

Kwamba Kitabu hicho kimelenga wanafunzi wa ngazi zote za kitaaluma. Dkt. Bakari ameeleza kama tutaweza kuwekeza kwenye TEHAMA tutaweza kutumia vyema fursa zilizopo.









Post a Comment

0 Comments