Na mwandishi wetu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 leo tarehe 16 Aprili, 2024.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Dennis Londo aliwasilisha pia taarifa ya Kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2023/24 pamoja na maoni na ushauri wa Kamati hiyo kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Makadirio hayo ya Ofisi ya Rais TAMISEMI yanatarajiwa kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge kwa muda wa siku tatu wakati huu wa Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge (Mkutano wa Bajeti) ambao umeanza Jumanne Aprili 2, 2024 na unatarajiwa kuhitimishwa Juni 28, 2024.
Hadi kufika Sasa Bunge limeshajadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizopo chini yake pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2024/2025.
0 Comments