Na mwandishi wetu
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Tanzania Bara,Abdulrahman Kinana ,amekemea vikali vitendo vya Ukabila,udini na ukanda,Ndani ya chama hicho,akiwataka wanachama kutambua kuwa hayupo ambaye anadhamana ya kukimiliki chama hicho.
Kinana ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara ambapo yupo kwenye ziara ya kukijenga chama.
Amesema ni vyema kwa watu wakatambua kuwa hakuna ukabila wala ukanda kwenye chama ni vyema wakaangalia mtu mwenye uwezo ,mwenye moyo wa kujitolea kuwatumikia wananchi na kuachana na dhana ya ukabila udini na ukanda.
“Naomba tumpime mtu kwa uwezo muhukumu mtu kwa uwezo wake kuna watu wanakaa Rorya awatoki hapa Bunda lakini ni watu wazuri na kama kuna kitu cha pekee ambacho Baba wa Taifa amekiacha ni watanzania kuwa wamoja na kuondoa tofauti zetu za ukabila usimuukumu mtu kwa ukabila na udini” Abdulrahman Kinana Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.
Aidha Kinana amesisitiza ni vyema kwa wanachama wakafuata misingi ya Mwl Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuwa akikemea masuala ya ukabila na aliwataka watanzania kuwa wamoja na wawe na mshikamano.
0 Comments