MKUU WA WILAYA YA MBINGA AZINDUA SEMINA YA MATUMIZI YA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022

 


Na mwandishi wetu

Mkuu wa Wilaya Mbinga *Mhe.Kisare Makori* leo tarehe 16-04-2024 amezindua semina ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na  makazi iliyofanyika mwaka 2022. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo Mbinga (FDC) na kuhudhuriwa    na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, dini na serikali kutoka ngazi ya mkoa na Halmashauri ya Mbinga Mji.


Akizindua semina hiyo *Mhe.Kisare Makori* amemushukuru *Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan* kwa kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kuratibu zoezi la sensa ya watu na makazi mwaka 2022, jambo ambalo limesaidia kupatikana kwa takwimu ambazo zinasaidia   kupanga mipango endelevu ya maendeleo.


 Alisisitiza kwamba takwimu za sensa ya watu na makazi zinatusaidia na zitatusaidia kuratibu, kupanga na kuainisha mipango ya maendeleo   kisekta katika wilaya ya Mbinga ili kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa uwiano.


Hivyo basi,  amewataka viongozi wa ngazi  mbalimbali katika wilaya  kutafsiri  takwimu hizo katika mipango mbalimbali ya maendeleo na utoaji wa huduma.


Semina hiyo ya uzinduzi wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi 2022 imeratibiwa na Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Mbinga Mjini  *Mhe.Jonas Mbunda* kwa kushirikiana na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Ruvuma Mhe.Mariam Nyoka pamoja na Ofisi ya Taifa Takwimu (NBS) Makao Makuu. 


Mwisho, Mkuu wa Wilaya alimpongeza Mhe. Jonas Mbunda, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini kwa kuratibu zoezi la semina na kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo la Mbinga Mjini kwa unyenyekevu , upendo na kujitolea katika kuwaletea maendeleo.






*imetolewa na*

*Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbinga*

*April 16, 2024*

Post a Comment

0 Comments