Mwanyekiti wa taasisi ya Mtetezi wa mama Geita Festo Haule akizungumza na waandishi wa Habari
Na,Joel Maduka,Geita….
Taasisi ya mtetezi wa Mama Wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita ,imetembelea na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa kwenye kituo cha afya cha Nyang’hwale huku wakipongeza huduma nzuri za afya ambazo zimeendelea kutolewa kwenye vituo na hospital zilizopo Wilayani Humo.
Akizungumza mara baada ya kuona na kujilizisha utolewaji wa huduma za afya kwenye kituo cha afya cha Nyang’hwale ,Mwenyekiti wa taasisi hiyo Festo Haule amesema wamelizishwa na namna huduma za afya zinavyotolewa kwa kina mama na watoto ambao wameshuhudia ubora wa miundombinu ulivyochangia kuboreshwa kwa huduma za afya.
“Huduma tumelizishwa nazo tumewaona wagonjwa hawana malalamiko yoyote ambayo yanahusu utolewaji wa huduma kwani kila mmoja wetu ameendelea kushukuru na kupongeza huduma bora zinazotolewa” Festo Haule Mwenyekiti wa Taasisi ya mtetezi wa Mama Wilaya ya Nyang’hwale.
Naye Katibu wa taasisi hiyo , Donald Yolamu,amesema miongoni mwa mambo ambayo wameyaona ni ujenzi wa jengo la upasuaji ambalo linajengwa kwenye Kituo hicho cha afya ambapo pindi litakapokamilika litasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa majengo.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho,Phinias Ndalo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wajumbe na viongozi wa taasisi ya Mtetezi wa Mama Wilaya ya Nyang’hwale kwa namna walivyoguswa na kuwatembelea wagonjwa.
0 Comments