BILIONI TATU (3) ZAKAMILISHA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA MOROGORO DC

 


Na mwandishi wetu


Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ina jumla ya Tarafa 6, Kata 31, Vijiji 149 na Vitongoji 733 pamoja na Watumishi wa Serikali 2776. 


Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilihamishwa kutoka Makao Makuu yaliyokuwepo Morogoro Mjini na kuhamishiwa Kata ya Mvuha KM 78 kutoka Morogoro Mjini ambapo jumla ya TZS 3,000,000,000.00 zilitengwa na Serikali kuu kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Jengo jipya la Utawala na sasa mradi umekamilika kwa 90% na kazi zilizobakia ni za nje.


Uongozi wa Halmashauri pamoja na wananchi wote tunamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha utawala bora ambao kwa sasa unapelekea utoaji wa huduma kwa wananchi kwa ukaribu zaidi, usimamiaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na ngazi za chini kwa ukaribu pamoja na kuchochea ukuaji wa haraka kiuchumi kwa wananchi wa Morogoro Vijijini.

Post a Comment

0 Comments