DK.MWINYI: KUZUNGUMZA NA WAJUMBE WA CCM MKOA WA KUSINI PEMBA.

 






Na mwandishi wetu


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewasili na kupokewa na Viongozi wa CCM wa Mkoa wa Kusini Pemba kichama, tayari kwa mazungumzo na Wajumbe wa Kamati za Siasa za Halmashauri kuu ya CCM ngazi ya  Tawi, Wadi, Majimbo, Wilaya na Mkoa.



Katika viwanja vya Tibirinzi Mkoa wa Kusini Pemba Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar  Ndugu Mohamed  Said Dimwa amewaongoza  viongozi wa CCM kumlaki Dk. Mwinyi alipowasili.



















📅 22 Agosti 2024

Post a Comment

0 Comments