EWURA YASHIRIKI TAMASHA LA KIZIMKAZI ZANZIBAR

 


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (Kushoto) alipotembelea banda la EWURA katika Tamasha la Kizimkazi linaloendelea Mkoa wa Kusini Unguja, Leo 24.08.2024. Kutoka kulia Kulia ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA Bw. Titus Kaguo, Ofisa Uhusiano Mwandamizi, Bi. Tobietha Makafu na Meneja Ufundi wa Petroli, Mha. Shaban Seleman.


Na mwandishi wetu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeshiriki katika Tamasha la Kizimkazi, linaloendelea katika kijiji cha Kizimkazi  Mkoa wa Kusini Unguja, lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraja la Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Agosti 18, 2024.


Katika tamasha hilo lenye kauli mbiu  ya ‘’ *Upishi Salama kwa Afya ya Mpishi na kwa Maendeleo ya Jamii”* EWURA inatoa elimu ya utekelezaji wa Sera ya Nishati ya mwaka 2015 pamoja na kutoa huduma kwa wananchi, hususani katika utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa mwaka 2024-2034.


Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Nishati zilizoshiriki katika tamasha hilo ni pamoja na TANESCO, PBPA, PURA, TPDC na REA.






Post a Comment

0 Comments