RAIS DKT SAMIA AAGIZA KUREJESHWA KWA HUDUMA ZA KIJAMII ZA ELIMU NA AFYA NGORONGORO

 




Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kurejeshwa kwa huduma za kijamii za elimu na afya katika Tarafa ya Ngorongoro, hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa kata 11 zilizopo Tarafa ya Ngorongoro waliokesha kwa siku 5 wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.


“Kila Diwani aende kwenye Kata yake afafanue huu ujumbe wa Mh.Rais Samia, Wananchi hawa waelezwe kwamba hamna aliyezuiwa kupigwa kura, Rais ameelekeza wapige kura kama Wananchi wengine”


“La tatu kubwa zaidi mabango haya yana ujumbe mwingi sana, Rais amenituma niseme ataandaa siku na mahali ambapo atakutana na Wawakilishi wa Jamii ya Ngorongoro ili mkamwambie Rais moja kwa moja, RC Makonda hakikisha unasimamia uamuzi wa Mh. Rais na kwamba vijiju vilivyopo vinabaki vilevile”


“La mwisho Mkurugenzi wa Ngorongoro nina habari kuna huduma hazitolewi vizuri, nakuagiza Mkurugenzi wa Ngorongoro, Rais anawapenda Watu wake, huduma zote zitolewe kikamilifu kote ambako zilisitishwa” ——— Lukuvi

Post a Comment

0 Comments