KIKWETE: RAIS SAMIA AFANIKISHA NDOTO YA MIAKA MINGI UUNDAJI WA BARAZA LA VIJANA LA TAIFA.

 



Na mwandishi wetu


_Baraza hili ni Mkombozi wa masuala ya Vijana kwa kusimamia sera kutatua kero zao._ 


Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete wiki hii wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa Agosti 12, 2024 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Jijini Dodoma.


"Namshukuru Mungu ndoto yetu tuliyoanza nayo Mwaka 2006 ya Uundaji wa Baraza la Vijana Taifa imefanikiwa baada ya leo kuzindua Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana 2007 Marekebisho ya 2024. Kwa hakika ukombozi wa Vijana umeanza kupatikana. Sera ikiwa ndiyo tochi kumulika tunakoelekea itasaidia utunzi wa sheria ambazo zitatatua baadhi ya Kero huku Wizara ikisimamia mabadiliko mengine kutengeneza msingi Bora wa Tanzania Tuitakayo." Aliandika Kikwete.





#VijanaTunajadili #KaziInaendelea

Post a Comment

0 Comments