Na mwandishi wetu
Wananchi wameipongeza Wizara ya Nishati kwa ufanisi wake katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa manufaa ya Taifa.
Pongezi hizo zimetolewa na wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti walipofika katika Banda la Wizara Ya Nishati kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea katika viwanja Vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma.
Mmoja wa Wananchi waliotoa pongezi hizo, Bw.Frank Stephen amesema Wizara imejitahidi kuhakikisha Nchini kunakuwa na umeme wa uhakika .
“Kwakweli mnajitahidi sana, sasa hivi tatizo la kukatika katika kwa umeme limemalizika, nawapongeza ila msibweteke tukajikuta tumerudi nyuma"
0 Comments