Na mwandishi wetu
TAMASHA la Utamaduni wa Mtanzania, Siku ya Jamii ya Wanyakyusa katika Kijiji cha Makumbusho ya Taifa,Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, limegusa hisia za wadau wengi hapa nchini ambao wametaka liwe endelevu.
Tamasha hilo lilianza jana, limefunguliwa na Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge,ambaye amesema litakuwa chachu ya kuiunganisha jamii ya wanyakyusa na kuunda chombo kitakacho simamia jamii hiyo.
“Nitasimamiaa kuunda chombo maalumu cha kutambua na kusimamia juhudi za jamii ya wanyakyusa. Tutashirikiana na Makumbusho ya Taifa na wadau mbalimbali kuona namna bora ya kufanya kuunda chombo hiki,”amesema Mwalunenge.
Mwalunenge,a,ameeleza chombo hicho kitakuwa na majumu mbalimbali yakiwemo ya kujadili changamoto na mafanikio ya wanyakyusa, hususan masuala ya elimu, fursa za maendeleo na maadili ya utamaduni.
Awali Chifu wa Wanyakyusa, Uswege Mwakabulufu, alisema tamasha hilo limetoa ujumbe mzito kwa jamii hiyo kuenzi utamaduni wake, huku akiwataka wana jamii kujikita katika kusomesha watoto na kufanya kazi kujiletea kipato.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mandalizi ya Tamasha hilo, Enelen Mwakapila,alisema, limehusisha, matukio mbalimbali, ikiwemo uzinduzi wa nyumba za asili za wanyakyusa katika Kijiji cha Makumbusho ya Taifa, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, chakula, mavazi, burudani za ngoma za asili , vinyaji na mavazi.
Katika tamasha hilo linalohitimishwa kesho, ngoma za asili za kinyakyusa za ing’oma ambazo ni Lugombo ya Wilaya ya Kyela na Kisiba ya Rungwe, zimekuwa kivutio kikubwa huku bendi ya muziki wa dansi ya Town Band ikiburudisha.
0 Comments