TANAPA Yaboresha Barabara za Serengeti kwa Ufanisi Zaidi

 







Na mwandishi wetu


Wadau wa utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti wameiomba Serikali kujenga barabara yenye tabaka gumu ili kudumu na kuondoa adha ya ukarabati wa mara kwa mara, kutokana na uharibifu unaosababishwa na idadi kubwa ya magari.


Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Nassoro Juma Kuji, akiwa katika ziara ya ukaguzi, aliagiza matengenezo ya haraka kwenye maeneo korofi na kusisitiza umuhimu wa barabara zinazopitika wakati wote. Pia alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada wa kifedha unaoendelea kuboresha miundombinu katika hifadhi za taifa.


TANAPA imesisitiza matumizi ya teknolojia mpya kujenga barabara zitakazodumu na kutatua changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi na idadi ya magari.

Post a Comment

0 Comments