CGF JOHN MASUNGA AKUTANA NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA

 



Na mwandishi wetu

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga tarehe 25 Oktoba, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na  Mhe. Chen Mingjian, Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Nchini Tanzania 

Viongozi hao wamejadili kuhusu masuala ya ushirikiano kati Tanzania na China jinsi Nchi hizo mbili zinavyoshirikiana katika mambo mbalimbali ili kuendeleza Uhusiano wa Kidiplomasia uliopa baina ya Mataifa hayo.

CGF Masunga amemshukuru Balozi huyo kwa kumualika pamoja na kuishukuru Serikali ya Watu wa China kwa kuendelea kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na kutupatia vifaa vya kuzima moto na uokoaji.

Aidha, CGF Masunga amemuomba Balozi huyo kupitia Nchi yake kuendelea kutoa nafasi zaidi za mafunzo pamoja na vitendea kazi kwani bado kuna uhitaji zaidi pamoja na ukuaji wa Sayansi na Teknolojia.

Naye Balozi Mingjian katika mazungumzo hayo, amesema ushirikiano kati ya Tanzania na China ulianza pale Tanganyika ilipopata uhuru na tumekuwa tukishirikia katika miradi mbalimbali ikiwemo mradi Mkubwa wa TAZARA

Pia Balozi huyo amefurahishwa na Kamishna Jenerali huyo kukubali mualiko wake na kupitia mazungumzo hayo amelifahamu vyema Jeshi hilo.

"Nitawasiliana na Makao Makuu ili kuona ni jinsi gani tunaweza kutoa ushirikiano katika Jeshi hili ikiwemo kuendelea kutoa mafunzo zaidi na vifaa vya Zimamoto na Uokoaji, amesema Mhe. Balozi Mingjian




Post a Comment

0 Comments