RAIS WA FEMATA BINA AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA FEMATA

 





🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥


*TAARIFA MUHIMU*

*TAREHE, 25/10/2024 DAR ES SALAAM*


Rais wa *FEMATA* na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya *FEMATA Mhe. John Wambura Bina* ameongoza kikakao cha Sekretarieti ya *FEMATA*.

Ametoa Mwongozo kuhusu Nidhamu, Maadili, Tabia njema kwa Viongozi wa Sekretarieti ya *FEMATA* na kuheshimiana, kupendandana na utii kwa kiapo cha katiba ya *FEMATA*.

Aidha Rais wa *FEMATA* aliongoza semina ya Maadili na Tabia njema kwa Viongozi wote wa sekretarieti ya *FEMATA* Ambapo Viongozi hao waliongozwa kupata kiapo cha Maadili na Utii.

Kiapo hicho ni muhimu kwa Viongozi wa Sekretarieti kwa kuzingatia Katiba ya *FEMATA* na ile ya *JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*.

Rais wa *FEMATA* kwenye semina elekezi hiyo alizigumzia mambo muhimu kabisa ya kimaadili, Nidhamu na tabia njema ya viongozi wa sekretarieti ya *FEMATA* kwa maslahi mapana ya serikali ya Muungano wa Tanzania, Wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa Madini Tanzania 🇹🇿 Wanaokadiriwa kuwa millioni sita nchini kote.


*WALIOHUDHURIA NI WAJUMBE WA SEKRETARIETI WAKIONGOZWA NA NDUGU, VICTOR TESHA MAKAMU WA RAIS FEMATA NA MWENYEKITI WA KAMATI ZA FEMATA, NDUGU, ROGERS SEZERO KATIBU MKUU WA FEMATA, NDUGU, PETER KABEPELA NAIBU KATIBU MKUU, SALUM RAMADHAN MSUYA MHAZINI MKUU, BI, JOYCE RAPHAEL KIRAHI NAIBU MHAZINI MKUU, DR. BERNARD JOSEPH MKURUGENZI WA HABARI NA MAHUSIANO YA KITAIFA NA KIMATAIFA FEMATA. WAJUMBE WAALIKWA KWENYE SEKRETARIETI YA FEMATA NI NDUGU, TARIQ JAMES KIBWE MWENYEKITI WA KAMATI YA MIRADI UWEKEZAJI NA UCHUMI, NA NDUGU, MAINA ANGELA OWINO MKURUGENZI WA SHERIA FEMATA*. 
















*IMETOLEWA NA KURUGENZI YA HABARI FEMATA

Post a Comment

0 Comments