Na mwandishi wetu
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI chini ya mwenyekiti wake Justin Nyamoga leo imeelekeza uongozi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume hiyo linaloendelea kujengwa hivi sasa liweze kukamilika kwa muda uliopangwa.
Mhe. Nyamoga ametoa maelekezo hayo katika majumuisho mara baada ya ziara yakutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Walimu makao makuu.
Amesema ukamilishwaji wa jengo hilo utaenda kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa Tume ya Utumishi wa Walimu katika kuwahudumia walimu wote nchini.
Aidha Mhe. Nyamoga amemtaka mkandarasi wa Jengo hilo ambaye ni JKT kuendelea kuzingatia thamani ya fedha katika ujenzi wa mradi huo ili kujenga jengo lenye ubora na litakalodumu kwa muda mrefu zaidi.
0 Comments