KCB BANK YAENDELEA KUOKOA MAISHA YA WATU WENYE SARATANI,WATOA ELIMU HII KUBWA.

 


Na mwandishi wetu


KCB Tanzania kwa kushirikiana na Maisha Wellness wametoa elimu kuhusu saratani kwa wafanyakazi na wateja wao.

Kampeni hii imelenga kuongeza ufahamu juu ya ugonjwa wa saratani na umuhimu wa uchunguzi wa mapema.

Kupitia zoezi hilo, walitoa vipimo vya afya kwa wafanyakazi na wateja, hatua ambayo inasaidia kugundua dalili za awali za saratani na kuwezesha hatua za haraka za matibabu.

Akizungumza na waandishi wa Habari mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Idara ha uendeshaji wa KCB Tanzania, Lulu Shikonyi alisema lengo lao ni kuboresha afya ya jamii kwa kutoa elimu na huduma za kinga dhidi ya saratani huku akiitaka jamii kuendelea na utamaduni wa kwenda kuangalia afya zao mara kwa mara .

“Tutakua na programu ambayo itakua inaangalia wanawake kwa upande wa saeatani na wanaume kwa upande wa saratani. Programu hiyo itakua inaendeshwa hapa ofisini kwetu na wateja wetu wote ambao watafika katika branch zote watakaribishwa kupata vipimo hivyo tukiwa hapa na madaktari na watoa elimu hiyo”

Aliongeza kuwa “Kama KCB tumeanza na hii ya kufundisha na kuwaelimisha wafanyakazi pamoja na wateja lakini hata mwaka jana tulikuwa na programu ya kutembelea hospitali ya Ocean road kwaajili ya kuwapa vifaa vidogo vidogo wale wagonjwa waliokuwepo kule hospitalini

Hivyo kwa kushirikiana na maisha wellness tunaweza pia tukaenda mbali zaidi kwa hizo huduma kwasababu wao wanaunga mkono programu hiyo pia watakuwa wanatupa maelekezo zaidi ni wapi tunapoweza kuweza kufanya udhamini”

Kwa upande wake, Meneja wa Uendeshaji kutoka Maisha Wellness, Dk. Hasitu Chakachaka, alisema kuwa upimaji wa mapema ni muhimu sana katika kugundua saratani katika hatua za awali. Alieleza kuwa endapo saratani itagundulika mapema, matibabu yake huwa na mafanikio makubwa. Hata hivyo, ikiwa ugonjwa huu utafumbuliwa kwa kuchelewa, saratani inaweza kusambaa mwilini na kufanya hali kuwa ngumu zaidi kutibu.

“Kinga ni bora kuliko tiba, ukifahamu mapema utafanya matibabu mapema na utaendelea vizuri bila tatizo lolote, msiogope kwani pia vipimo vyao ni rahisi sana”

Post a Comment

0 Comments