MNAZI MMOJA KUMEANZA KUCHANGAMKA
DC MPOGOLO AITA WATU MIKOPO YA BILIONI 14
MAANDALIZI yanaendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, ambapo Mkuuwa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kongamano la wazi kuhusu elimu ya mikopo ya asilimia 10 inayotarajiwa kuanza kutolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Kongamano hilo la sikumbili linaanza kesho katika viwanja hivyo litahusisha pia elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
, Mpogolo amesema kiasi cha sh. bilioni 14 kimetengwa na halmashauri hiyo kwa ajili ya mikopo hiyo kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na wenye ulemavu.
Ameeleza , kongamano hilo litahusisha elimu ya namna ya kuunda vikundi, matumizi sahihi ya fedha za mikopo, utaratibu na marejesho.
“Rais Dk. Samia, ameruhusu mikopo hii itolewe. Tutatoa kwa utaratibu mpya kupitia benki hivyo elimu ya fedha ni muhimu kutolewa kabla mwananchi hajakopeshwa,”ameeleza Mpogolo.
Amesema katika kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Amo Foundation ‘Vijana Kazini’, itahusisha maonesho ya wajasiriamali wakati na wadogo.
Ameeleza, konganano hilo pia litatumika kuwasajili watu wanaostahili kupata mikopo hiyo katika daftari maalumu.
“Pia tutatoa majiko ya nishati salama kwa mama na baba lishe kuunga mkono sera ya Rais Dk. Samia katika matumizi ya nishati hiyo,”amebainisha Mkuu huyo wa Wilaya.
Mewahimiza wananchi wenye nia ya kupata mikpo kujitokeza kwa wingi ndani ya siku hizo mbili.Kongamano hilo litafungwa Novemba 12 na Naibu Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu.
0 Comments