Na mwandishi wetu
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeshiriki katika uzinduzi wa filamu ya Amazing Tanzania pamoja na maadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika tarehe 4 Novemba, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo adhimu na la kihistoria ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb) huku ujumbe wa China ukiwakilishwa na Makamu Waziri wa Utalii na Utamaduni Mhe. Lu Yingchuan.
Uzinduzi wa filamu ya Amaizing Tanzania na maadhimisho ya miaka 60 ya Kidiplomasia ni hatua muhimu kufuatia juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, kutangaza na kukuza utalii pamoja na kufungua fursa za uwekezaji kati ya Tanzania na China.
Aidha, uzinduzi wa Filamu ya Amazing Tanzania ni jukwaa muhimu katika kutangaza urithi wa kipekee na vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na kufungua milango zaidi kwa watalii na wawekezaji kutoka China, bara la Asia ulimwenguni kwa ujumla.
Takwimu za watalii kutoka China wanaotembelea Tanzania zinaonesha kuwa mwaka 2018 kabla ya Uviko-19 watalii kutoka China waliotembelea Tanzania ni takribani 32,000, baada ya uzinduzi wa filamu ya Amaizing Tanzania mwezi Mei, 2024 idadi imeendelea kuongezeka ambapo hadi kufikia Septemba 2024 zaidi ya Wageni 54,000 kutoka nchini China wametembelea vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania
Ujumbe wa NCAA ukiongozwa na mwakilishi wa Kamishna wa Uhifadhi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Gloria Bideberi
katika maadhimisho hayo umenadi vivutio vya utalii , shughuli za uhifadhi, vivutio vya malikale pamoja na fursa za uwekezaji vilivyopo hifadhi ya Ngorongoro kwa wageni mbalimbali waliohudhuria tukio hilo.
0 Comments