Na mwandishi wetu
LICHA ya Serikali kufanya jitihada za kuinua uchumi,Tatifiti inaonesha bado kiwango cha umasikini nchini ni mkubwa.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Dkt Lucas Katela ni Mkurugenzi wa Utafiti na mafunzo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umaskini (Repoa) wakati wa uwasilishaji wa Utafiti kuhusu hali ya uchumi nchi,ambapo ulijikita kuangalia maoni ya wananchi wanavyoona kuhusu hali ya uchumi.
Dkt Katela,amesema asilimia 38 ya wananchi wanasema wanaumasikini wakipato huku ikiwa tofauti na mwaka 2022.
"Maeneo ya vijijini kwenye utafiti wetu ,wamekuwa wakilalamikia umasikini wa kipato ambayo imechangiwa na changamoto ya miundombinu ambapo bidhaa wanazozalisha zinashindwa kusafirishwa"Amesema Dkt Katela.
Hata hivyo Dkt Katela,amesema katika utafiti huo imeonesha kuna jitihada kubwa za Serikali kuboresha maeneo mbalimbali huku jitihada hizo zikitakiwa kuongezwa.
Dkt Katela,amesema katika utafiti huo umeonesha hali ya ulinzi nchini umeimarika,ujenzi wa miundombinu imeimarika,huduma
za kijamii ikiwemo Afya,shule zimeimarika.
"Katika utafiti huu wananchi wamependekeza kwa serikali imetakiwa kuongeza nguvu ikiwemo Elimu,maji,masuala Afya ili kusaidia kupunguza umasikini"
Kwa Upande wake Mtafiti mwandamizi kutoka Repoa,Profesa Pascal Miho,amesema serikali kufanya kazi kubwa wananchi wanataka iongeze juhudi kwenye masuala ya miundombinu,Afya wananchi wametaka iongeze juhudi kwani itasaidia kupunguza umasikini.
0 Comments