Na mwandishi wetu
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeomba radhi kwa abiria wa treni ya mchongoko (EMU) walioanza safari yao Dar es salaam kwenda Dodoma leo November 03,2024 saa 2:00 asubuhi na kusimama ghafla majira ya saa 2:20 kati ya Pugu na Soga.
TRC imeomba radhi pia kwa abiria wa treni ya saa 11:15 alfajiri kutoka Dodoma na treni ya saa 3:30 asubuhi kutoka Dar es salaam ikijumuisha safari nyingine za siku ya leo ambazo zimeathiriwa kufuatia hitilafu kwenye mifumo ya uendeshaji.
“Mafundi wetu wako eneo la tukio wanafanyia kazi changamoto hiyo, tutaendelea kuwapatia taarifa, tunatanguliza shukrani”
0 Comments