WAZAZI WAMSHUKURU MBUNGE MAVUNDE KWA UJENZI WA UZIO SHULE YA MSINGI UHURU-DODOMA

 




*WAZAZI WAMSHUKURU MBUNGE MAVUNDE KWA UJENZI WA UZIO SHULE YA MSINGI UHURU-DODOMA*


▪️Shule ina umri wa miaka 96 tangu kuanzishwa kwake


▪️Muingiliano wa masomo na biashara kuzunguka Shule ilikuwa kikwazo


▪️Wanafunzi washukuru kuhakikishiwa Usalama wao


▪️Mbunge Mavunde amshukuru Rais Samia kwa madarasa


📍Dodoma

Wananchi na wazazi wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Jijini Dodoma, wamempongeza na kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh. Anthony Mavunde* kwa ufadhili wa ujenzi wa uzio wa shule hiyo ili kuboresha mazingira rafiki ya wanafunzi kusomea tofauti na awali ambapo muingiliano ulikuwa mkubwa kati ya wafanyabiashara wanaozunguka eneo la shule na shughuli za masomo za wanafunzi.

Wakitoa shukrani zake leo wakati wa hafla ya kukabidhi uzio huo,Mwenyekiti wa Kamati ya wazazi wa Shule ya Uhuru *Ndg. Aman Sadick* na Mwenyekiti wa CCM kata  *Ndg. Rashid Said Gwazae* wamesema moja ya changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili wanafunzi katika eneo hilo ni juu ya usalama wao na kukosa utulivu wakati wa masomo na hivyo kumshukuru Mbunge Mavunde kutatua kero hii iliyodumu kwa miaka mingi ndani ya  miaka 96 ya maisha ya shule hiyo kwa kuwa Shule ya Uhuru ipo katikati ya shughuli nyingi za kibiashara na kijamii.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh. Anthony Mavunde* amemshukuru Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuboresha miundombinu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ya shule hiyo kongwe ya Uhuru.

“katika kuunga mkono jitihada hizi kubwa za serikali niliona ni vyema mimi na wadau wengine wa maendeleo tuungane kujenga uzio wa shule ili kupunguza changamoto katika eneo hili.

Kumekuwepo na vijana wanaovuta gundi na bangi,pia kumekuwepo na vitendo vingi visivyo vya kimaadili  katika eneo la shule kwa kukosa uzio.Hivyo uwepo wa uzio utakuwa suluhu ya changamoto nyingi”Alisema Mavunde

Naye Diwani wa Kata ya Uhuru *Mh. Khalfan Kabwe* amesema ilikuwa ni hitaji kubwa kwa wananchi wa uhuru kuona wanafunzi wa Shule ya Uhuru wanalindwa na kulelewa katika maadili mema,hivyo ujenzi wa uzio huo uliofadhiliwa na Mbunge Mavunde utabaki kama kielelezo na alama ya utumishi mwema ambayo haitafutika kamwe kwa wanafunzi na wazazi wa Uhuru










Post a Comment

0 Comments