"ANDAENI MUONGOZO WA UKAMILISHA WA UJENZI WA SHULE YA MKOA YA WAVULANA KATAVI” MHE. NYAMOGA

 




OR-TAMISEMI, Katavi

Kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI ikiongozwa na mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Justin Lazaro Nyamoga imeuelekeza uongozi wa mkoa wa Katavi kuandaa muongozo wa ukamilishaji wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya wavulana Katavi iliyoko wilaya ya Mpanda kwa kuzinganitia ushauri wa kitaalamu.

Mhe. Nyamoga ametoa maelekezo hayo katika kikao Cha majumuisho ya ziara ya Kamati hiyo katika mkoa wa Katavi baada ya kutembelea mradi huo unaoendelea na ujenzi.

“Tunatarajia tupate taarifa ya utekeleza wa mpango huo na vizuri Wizara ikasimamia kwasababu ni mradi wa fedha nyingi ili tusiingie kwenye mkwamo hiyo itakuwa vizuri lakini sisi tutatarajia taarifa ya utekelezaji wa taarifa yetu wakati wa bajeti”. Amesema

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amepokea maelekezo hayo na kuahidi kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ujenzi wa shule hiyo

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko ameahidi kuongeza wigo wa usimamizi ili shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule saba nchini zinazojengwa na mradi wa SEQUIP unakamilika kwa kuzingatia viwango.







Post a Comment

0 Comments