Na mwandishi wetu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameongoza kikao kilichoikutanisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jeshi la Polisi Tanzania pamoja na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kujadili na kuweka mikakati ya kuzuia ajali za barabarani nchini.
Kikao hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi ya kuongeza mikakati ya kuzuia ajali zinazosababishwa na makosa ya uzembe.
Pamoja na mambo mengine, wamejadili utaratibu wa utoaji wa leseni kwa madereva pamoja na kuweka mikakati ya pamoja kwa Jeshi la Polisi na LATRA ya kupambana na kuzuia ajali za barabarani.
Kikao hicho kimefanyika Dodoma, leo Januari 06, 2025 ambapo kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura na Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa barabara (LATRA), DCP Johansen Kahatano pamoja na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara na Jeshi la Polisi.
0 Comments